LIVERPOOL WAANZA KUMPOTEZEA KOLO TOURE.
Majogoo wa jiji Liverpool huenda wakampa mkono wa kwaheri beki wa
kati kutoka nyumbani Afrika katika nchi ya Ivory Coast Habib Kolo Toure,
kufuatia uongozi wa klabu hiyo kushindwa kuonyesha dalili zozote za .....
kumsainisha mkataba mpya mpaka sasa.
Mkataba wa beki huyo mwenye umri wa miaka 34, utafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, hali ambayo inaonyesha dhahir huenda mambo yakawa magumu kwake na kuanza kusaka mahala pengine pa kumalizia soka lake.
Hata hivyo Toure, bado ana matarajio makubwa ya kusainishwa mkataba mpya ambao utamuwezesha kuendelea kuitumikia klabu ya Liverpool, japo dalili zinazoonekana kuonyesha wazi huenda akashindwa kutimiza matarajio hayo.
Beki huyo ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Arsenal pamoja na Man city kabla ya kuelekea mjini Liverpool mwaka 2013, amesisitiza kuwa na mahusiano mazuri na viongozi wa The Reds hivyo hana shaka na mustakabali wake klabuni hapo.
Mpaka sasa Kolo Toure ameshaitumikia Liverpool katika michezo 30 na hajabahatika kufunga bao.

0 comments: