CHARLIE CHAPLIN ALIAMUA KUOA KUEPUKA KIFUGO

Ripoti ya siri inayoonyesha kwamba aliyekua mchekeshaji maarufu duniani Charlie Chaplin angeozea jela kama asingemuoa Lita Grey imegundulika.
Ripoti hiyo yenye kurasa hamsini inaonyesha kwamba Chalrie alikutwa na kosa na kumpa ujauzito msichana Lita Grey akiwa chini ya umri wa miaka 18.
Charlie alieleza kwamba alimtamani msichana huyo tangu
akiwa na miaka 8 lakini alikutana nae kwenye filamu aliyomshirikisha kipindi hicho msichana huyo akiwa na umri miaka 15 huku yeye akiwa na umri wa miaka 35.
Charlie alianzisha uhusiana na binti huyo ambapo alimpa ujauzito na Mama wa binti huyo alipogundua alimshtaki Charlie katika kituo cha polisi. Hata hivyo shtaka hilo liliisha kwa sharti la Charlie kukubali kumuoa Lita la sivyo angeenda jela.
Charlie na Lita walifunga ndoa mwaka 1924 tarehe 25 November, na kubahatika kuzaa nae watoto wawili wa kiume.
Muigizaji huyo alifariki mwaka 1977 huku ripoti zikionyesha kwamba aliwahi kukiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi takribani na wanawake elfu 2.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...