PESA ZA MKIMBIZA KHALID CHOKORAA KUGOMBEA UDIWAI BAGAMOYO.

Muimbaji na Rapa wa Bendi ya Mapacha Watatu Khalid Chokoraa amesema ameachana na mpango wake wa kugombea Udiwani kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu kutokana na ukata wa pesa.
Khalid Chokoraa amesema
‘Nilikua na mpango wa kugombea Udiwani huko kwetu Bagamoyo lakini nimeshindwa kufanya hivyo sababu ya pesa ndugu yangu”.
Chokoraa alifafanua kwa kusema kwamba gharama za mchakato mzima wa siasa kwa sasa unahitaji pese. Mwanamziki mwanachama wa chama cha mapinduzi ccm ambae pia ni Mwanamasumbwi mpaka sasa ameshapigana mapambano mawili na kushinda yote huku akiomba wadau wa ndondi kumuandalia pambano jingine.
Kuhusu upande wa bendi yo ya mapacha watatu, Chokoraa amesema tayari wameachia wimbo wao mpya unaoitwa naonewa waliomshirikisha Mkali wa bongo flava Ali Kiba. Kuhusiana na tetesi za kutaka kurudi Twanga, Chokoraa alisema si kweli na kwa sasa hanampango huo kwani bendi yao inafanya vizuri na wapo imara.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...