PFA YAWACHONGANISHA WACHEZAJI ENGLAND

Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard pamoja na mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane wamejikuta wakipambanishwa katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England PFA.
Hazard anarejea katika orodha hiyo ikiwa ni mara yake ya pili mfululizo baada ya kuorodheshwa msimu uliopita, lakini hakufanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu baada ya kuachwa mbali na aliyekua mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez.
Hii ni mara ya kwanza kwa Harry Kane kuingia katika orodha
hiyo kutokana na kufanya vizuri katika msimu huu akiwana klabu yake ya Spurs ambapo mpaka sasa ameshafanikiwa kuifungia klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London mabao 29.
Kane, ni mchezaji pekee kutoka nchini England aliyeorodheshwa kwenye orodha ya wanaowani kinyang’anyiro hicho, huku sifa kubwa inayombeba ni ufungaji wa mabao 19 katika ligi ya nchini hiyo akiwa sawa na mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, ambaye pia amejumuishwa.
Mabingwa watetezi wa ligi ya nchini England Man city, hawajabahatika kuingiza mchezaji yoyote kwenye orodha ya wanaowani tuzo za PFA msimu huu, hali inyodhihirisha mambo yalikua mabaya kwao kwa mchezaji mmoja mmoja, licha ya mshambuliaji wao Sergio Aguero kuwa katioka orodha ya wafungaji waliofikisha mabao 19 katika ligi.
Katika orodha kamili ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa msimu ya PFA yupo Diego Costa (Chelsea), David de Gea (Manchester United), Philippe Coutinho (Liverpool), Eden Hazard (Chelsea), Harry Kane (Tottenham Hotspur) pamoja na Alexis Sanchez (Arsenal).
Kwa upande wa wanaowani tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa msimu mwenye umri mdogo yupo Thibaut Courtois (Chelsea), Philippe Coutinho (Liverpool), David de Gea (Manchester United), Eden Hazard (Chelsea), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Raheem Sterling (Liverpool).
PFA pia wametoa orodha ya wachezaji wanawake wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa msimu ambapo yupo
Eniola Aluko (Chelsea), Lucy Bronze (Manchester City), Jess Clarke (Notts County), Karen Carney (Birmingham City), Kelly Smith (Arsenal) pamoja na Ji So-yun (Chelsea)
Wanaowani tuzo ya mchezaji bora chipukizi upande wa wanawake yupo Freda Ayisi (Birmingham City), Hannah Blundell (Chelsea), Aoife Mannion (Birmingham City), Nikita Parris (Manchester City) pamoja na Leah Williamson (Arsenal)

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...